Ihre Browserversion ist veraltet. Wir empfehlen, Ihren Browser auf die neueste Version zu aktualisieren.

Karibu katika tovuti yetu mpya ya ASCENSOR!

Tunatumai utapata habari nyingi za muhimu kupitia tovuti yetu.Ubora wa kazi zetu na mafanikio ni muhimu sana kwetu sisi na kwako pia.

 

Unaweza pia kupata undani wa habari zetu kupitia mtandao au unaweza pia kuwasiliana na kundi letu la huduma kwa wateja ili kupata huduma zetu.

Tumeamua kubuni tena mzee yetu. Kwa hoja zetu kuhusu nguvu mbadala, photovoltaic(PV),huduma za kijani na usindikaji wa taka,temembelea tovuti yetu mpya kwenye

 

RUNICA AFRICA

 

na pia unaweza kupata kwenye LinkedIn.

Katika uwasilishaji wa ASCENSOR tutajishughulisha na mandhari ambayo wanawake wanapitia na changamoto mbalimbali sanasana hapa Africa tutawasaidia tuwezavyo.
Unaweza pia kutupata kwenye Facebook na Twitter, hivi karibuni tutakua pia kwenye mitandao mingine kama IM, Messenger, Twitter, whatsapp, WeChat, Skype, Telegram na Threema.

Tunampango wa kuanzisha kampuni nyengine miezi ya hivi karibuni katika Afrika Mashariki.Katika utafutaji wetu wa wafanyakazi waliobobea,tilikutana na kundi la wazungu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na pia kuwarubuni wanawake wa kiafrika kutumia njia mbalimbali.Hapa pia sisi hutoa msaada wa bure kwa wanawake hao waliokutwa na majanga haya.
Kesi nyengine za awali zimenihusisha na nimeamua kuchukua hatua kuwasaidia hawa wanawake wa kiarfica waliyorubuniwa.Kwa upande mwingine tungependa pia kutoa msaada na mwelekeo kwa wanawake wa kila umri kuzuia vurugu na unyanyasaji.Pia tungependa kuwapa moyo wanawake waliyonyanyaswa kupata msaada wenye uhakika.Haijalishi mtu yupo umbali gani badol anaweza kuupata msaada huu.
itambulike kua msaada wetu katika hili swala ni bure kabisa bila malipo yoyote.

Hapa tunataka kutofautisha kati ya vurugu na wanawake kutumiwa vibaya.
Vurugu au unyanyasaji wa wanawake pia haijaripotiwa vilivyo .Kuenea kwa tatizo hili sugu linasababishwa na kulionea aibu,ukosekanaji wa vitenda kazi na hata kukubaliana kinyonge na swala hili.
Wanawake wengi wanaonyanyaswa hua hawatoi taarifa katika sehemu husika zinazotoa huduma hizi.

Anagalizo muhimu sana kuhusu usalama wa taarifa zako unazozitoa za kibanafsi na taarifa tunazopata pia.
Taarifa zote tutazishughulikia kwa usiri mkubwa sana.Hatutawai kutoa taarifa hizo bila ya ridhaa yako katika vyombo husika na kwa watu wengine.

Taarifa nyengine na anwani zitachapishwa hivi karibuni

Tunatoa huduma za bure na huduma nyengine kwa wanawake wote duniani. Pia tunasaidiana na mashirika na watu mbalimbali.